Google imejitolea kukusaidia kugundua mazingira yako. Picha zilizo kwenye huduma zetu zinakusudiwa kuboresha hali yako ya utumiaji, kwa kukusaidia kukagua na kugundua maeneo yaliyo karibu na wewe au duniani kwote. Tunajitahidi kuhakikisha kwamba picha hizo ni muhimu na zinaonyesha uhalisia wa ulimwengu ambao watumiaji wetu huchunguza.

Picha za Taswira ya Mtaa zinaweza kuchangiwa na washiriki wa nje au Google. Unaweza kujua tofauti kwa jina au aikoni ya maelezo iliyo kwenye kila picha. Picha iliyopigwa na mchangiaji wa nje na kuchapishwa kwenye Ramani za Google ni mali ya mchangiaji huyo (au mtu mwingine yeyote atakayemkabidhi).

Ukurasa huu unafafanua Sera ya Picha za Taswira ya Mtaa Zinazochangiwa na Google. Ili uone sera zinazohusiana na maudhui yanayochangiwa na mtumiaji, tafadhali angalia Sera ya Maudhui ya Ramani Yanayochangiwa na Watumiaji.

Sera ya Picha
ya Taswira ya Mtaa Inayochangiwa na Google

Ili kusaidia kuhakikisha kwamba kila mtu anayetazama picha za Taswira ya Mtaa anapata hali nzuri na bora ya matumizi, tumebuni Sera ya Maudhui ya Taswira ya Mtaa Yanayochangiwa na Google. Sera hii inaelezea jinsi tunavyoshughulikia maudhui yasiyofaa na vigezo muhimu vya kuchapisha picha za Taswira ya Mtaa kwenye Ramani za Google. Tafadhali pitia sera yetu mara kwa mara, kwani huenda tukairekebisha.

Picha za Taswira ya Mtaa si za Moja kwa Moja

Picha za Taswira ya Mtaa huonyesha tu yale ambayo kamera zetu ziliona wakati wapigapicha wetu walipopita katika eneo husika. Baadaye, hutuchukua miezi kadhaa kuzichakata. Hii inamaanisha kwamba maudhui unayoona yanaweza kuwa ya miezi au miaka kadhaa iliyopita. Katika baadhi ya maeneo ambapo tumekusanya picha kwa miaka mingi, unaweza pia kuangalia mabadiliko katika picha hizo kwenye kipengele chetu cha Zana ya Kuonyesha Wakati.

Kutia ukungu

Google huchukua hatua kadhaa ili kulinda faragha ya watu binafsi wakati picha za Taswira ya Mtaa zinachapishwa kwenye Ramani za Google.

Tumetengeneza teknolojia ya kisasa ya kutia ukungu kwenye nyuso na nambari za magari na inatumika kutia ukungu kwenye nyuso na nambari za magari zinazoweza kutambulika, katika picha zinazochangiwa na Google kwenye Taswira ya Mtaa. Iwapo utaona uso wako au nambari ya gari lako inahitaji kufunikwa zaidi kwa kutia ukungu au kama ungependa tukufunike au tufunike nyumba yako au gari lako kabisa, wasilisha ombi kwa kutumia zana ya "Ripoti tatizo".

Maudhui Yasiyofaa

Unaweza kuripoti maudhui yasiyofaa kwa kutumia kiungo cha "Ripoti tatizo". Tunachukulia aina zifuatazo kuwa maudhui yasiyofaa isipokuwa pale ambapo kuna thamani ya kisanii, elimu au ya hali halisi katika maudhui.

Ukiukaji wa haki za uvumbuzi

Ukiukaji wa haki za uvumbuzi

Haturuhusu picha au maudhui mengine yoyote yanayokiuka haki za kisheria za mtu mwingine ikiwa ni pamoja na hakimiliki. Kwa maelezo zaidi au kutuma ombi la DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali), kagua taratibu zetu za hakimiliki.

Aikoni ya maudhui yanayoonyesha ngono waziwazi

Maudhui yanayoonyesha ngono waziwazi

Haturuhusu maudhui dhahiri ya ngono.

Aikoni ya maudhui haramu, hatari au ya vurugu

Maudhui haramu, hatari au ya vurugu

Haturuhusu maudhui yanayokiuka sheria, yanayochochea vitendo hatari au vya kihalifu au yenye picha za kutisha au vurugu iliyokithiri.

Aikoni ya Unyanyasaji na vitisho

Unyanyasaji na vitisho

Haturuhusu maudhui yanayotumia Taswira ya Mtaa kunyanyasa, kuchokoza au kuwashambulia watu.

Matamshi ya chuki

Matamshi ya chuki

Haturuhusu maudhui yanayochochea au kuruhusu vurugu dhidi ya watu binafsi au makundi ya watu kwa misingi ya mbari au asili ya kikabila, dini, ulemavu, jinsia, umri, uraia, hali ya kuwahi kuwa mwanajeshi, mwelekeo wa kingono au utambulisho wa kijinsia.

Aikoni ya Maudhui ya Ugaidi

Maudhui ya Ugaidi

Haturuhusu mashirika ya kigaidi kutumia huduma hii kwa madhumuni yoyote, ikiwemo kusajili wanachama. Tutaondoa pia maudhui yanayohusiana na ugaidi kama vile maudhui yanayoendeleza matendo ya kigaidi, kuchochea vurugu au kutukuza mashambulizi ya kigaidi.

Aikoni ya Uhatarishaji wa watoto

Uhatarishaji wa watoto

Google ina sera ya kutoruhusu kabisa maudhui yanayowatumia watoto vibaya au kuwanyanyasa. Hii ni pamoja na picha za unyanyasaji wa ngono na maudhui yote yanayowaonyesha watoto kwa njia ya ngono. Ukipata maudhui yoyote unayofikiria yanawanyanyasa watoto kwa njia hii, tafadhali usiyashiriki tena au kuandika maoni, hata kama nia yako ni kuiarifu Google. Ukipata maudhui mahali pengine kwenye wavuti, tafadhali wasiliana na Kituo cha Kitaifa cha Watoto Walipotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) moja kwa moja.

Aikoni ya Maelezo ya binafsi yanayomtambulisha mtu

Maelezo ya binafsi yanayomtambulisha mtu

Haturuhusu maudhui yaliyo na maelezo ya binafsi yanayomtambulisha mtu kama vile maelezo ya kadi za mikopo, rekodi za matibabu au kitambulisho kilichotolewa na serikali — iwe maelezo ni yako au ya mtu mwingine.