Ajiri mtaalamu wa kuaminika, uboreshe uonekanaji wako

Ajiri mtaalamu wa kuaminika, uboreshe uonekanaji wako

Watch the film

Link to Youtube Video (visible only when JS is disabled)

Wataalamu wa kuaminika wa Taswira ya Mtaa ni:

Aikoni ya Mtaalamu wa Kuaminika
  • Wapokeaji wa beji ya kuaminika ya Taswira ya Mtaa
  • Wachangiaji wa kipekee walio na Picha hamsini za digrii 360 zilizoidhinishwa na kuchapishwa
  • Wanaoangaziwa katika orodha yetu ya wataalamu wa kuajiriwa
  • Wanaoweza kutumia bidhaa za chapa za Kuaminika kwa malengo ya uuzaji

Mambo unayoweza kutarajia kutoka kwa mtaalamu

Kwa biashara inayotaka kujulikana, mchangiaji maarufu wa Taswira ya Mtaa anaweza kuisaidia ionekane na itambulike kwenye Ramani za Google. Lakini kabla uanze, ni muhimu uelewe jukumu la kila mshirika katika shughuli hii.

Wamiliki wa biashara

  • Ikiwa utaajiri mpigapicha anayeaminika katika Taswira ya Mtaa ili apige picha za biashara yako, tafadhali kumbuka kuwa Google haiwezi kukuhakikishia ubora wa huduma yake.
  • Majadiliano yote kuhusu sheria na masharti, huduma na bei ya kupiga picha yatakuwa kati yako na mpigapicha.
  • Malipo yoyote ya onyesho la mtandaoni au picha yanapaswa kulipwa kwa mpigapicha anayeamika katika Taswira ya Mtaa - hakuna malipo yanayofanywa kwa, au kupitia Google.
  • Ikiwa kutakuwepo na mzozo, utahitaji kuusuluhisha na mpigapicha au kampuni kulingana na sheria na masharti ya mkataba wenu.
  • Kama ungependa kuripoti tatizo linalohusu huduma zinazotolewa na mpigapicha anayeaminika wa Taswira ya Mtaa, unaweza kufanya hivyo kwa kujaza fomu hii.
Mmiliki wa biashara kwenye Taswira ya Mtaa ya Google na mtaalamu wa kuaminika

Kupata huduma za Taswira ya Mtaa

Kwa kutumia teknolojia ya Street View ready, wataalamu wa kuaminika wanaweza kupiga na kuchapisha picha za mtaa ili kusasisha Taswira ya Mtaa katika jumuiya zako.

  • Hata kama Google haiajiri wapigapicha au kampuni za kupiga picha, huwa tunaruhusu wachangiaji wachapishe picha zilizosasishwa za barabara kwenye Taswira ya Mtaa. Orodha yetu maalum ya wataalamu wa kuajiriwa inaonyesha wapigapicha na kampuni ambazo zilionyesha ustadi kwa kuchangia picha maridadi zenye ubora wa juu.
  • Google inaendelea kujitahidi kusafiri katika nchi nyingi ili kukuletea picha ambazo zinaboresha hali yako na zinazokusaidia ugundue mazingira yako. Angalia tunakoelekea ili uone iwapo tutakuja mahali ulipo hivi karibuni, au uwasiliane na mtaalamu wa kuaminika iwapo ungependa kuwa na picha mpya badala ya kusubiri hadi wakati huo.
Mtaalamu wa kuaminika wa Taswira ya Mtaa ya Google na kamera

Tafuta mtaalamu wa kuaminika katika eneo uliko

Anza kwa kutafuta mtaalamu wa kuaminika aliye karibu.

Wakala Jiji Barua pepe Nambari ya Mawasiliano
Wakala Jiji Barua pepe Nambari ya Mawasiliano

*Uandikishaji wa wataalamu wapya kwenye Mpango wa wapigapicha wanaoaminika katika Taswira ya Mtaa umefungwa kwa muda.