Thrive DC

Shirika la Thrive DC lilianzishwa 1979 na linafanya kazi ya kuzuia na kumaliza tatizo la ukosefu wa makazi mjini Washington, D.C.

Kiasi cha Utendaji

Ndogo

Sekta

Huduma za Misaada ya Kibinadamu

Malengo

Andikisha, funza na uwasiliane na watu wanaojitolea

Changisha pesa

Hamasisha

Ongeza tija na uboreshe shughuli

Panua hadhira yako

Pata wafadhili

Vutia watu wanaotembelea tovuti yako

Wasiliana na ushirikiane kwa njia bora zaidi

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Aliyepiga Picha

Thrive DC

Tovuti

https://www.thrivedc.org

Changamoto

Asilimia 16.4 ya idadi ya watu mjini Washington D.C. wanaishi katika umaskini1 ilhali bei za nyumba zinaongezeka kila mwaka. Shirika la Thrive DC linahitaji kuchukua hatua haraka ili kukabili hatari inayoongezeka ya ukosefu wa makazi jijini D.C., ambayo kwa sasa inaathiri watu 7,4002.

“Wakati unachangisha dola milioni 3 ili kutoa maelfu ya vyakula kwa mwaka, kuwasaidia watu wawe watulivu, warudi kutoka vifungo vya jela au wapate kazi, kitu ambacho hungependa kuona ni matokeo duni. Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida hutusaidia kupata matokeo bora.”

Daniel Meloy, Mkurugenzi wa Maendeleo katika Shirika la Thrive DC.

Simulizi

Asubuhi ya kawaida katika shirika la Thrive DC huanza kwa kuwapa watu 150-200 kiamsha kinywa kwa upendo, ambapo wateja pia wanaweza kufikia vifaa vya kuosha nguo na kuoga. Wiki nzima, shirika la Thrive DC hupanga ushauri kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, mipango ya kuwapokea na kuwasaidia waliotoka kizuizini, hifadhi ya chakula, mafunzo kuhusu ujuzi wa kazi, ufikiaji wa maabara ya kompyuta na huduma ya kutuma barua kwa wateja 1,000. Shirika la Thrive DC lina wafanyikazi 16 pekee na kila mwaka huwahudumia zaidi ya wateja 2,000, husimamia watu 2,400 wanaojitolea, hutoa vyakula 160,000 na husambaza zaidi ya ratili 140,000 ya vyakula kupitia stoo ya chakula cha dharura.

Mbinu zao za ufanisi ni pamoja na timu yenye bidii, mfumo uliopangwa vyema wa kusimamia watu wanaojitolea na mikakati bora ya kuchangisha. Wakati timu yetu ya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ilitembelea ofisi ya shirika la Thrive DC mjini Washington, tulijivunia kuona jinsi bidhaa zetu zinawafurahisha!

Matokeo bora ni muhimu kwa wafanyakazi wachache ambao kazi yao hubadilisha maisha ya maelfu. Google Workspace husaidia shirika la Thrive DC kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi. Kalenda ya Google hutumika kuwaweka mamia ya watu wanaojitolea katika mipango sita tofauti kila wiki. Matukio hupakwa rangi ili kuona kwa muhtasari vikundi ambavyo vimejitolea wakati mahususi. Hifadhi ya Google na Meet zinaboresha ushirikiano: "Tunapopanga hifadhidata yetu ya wanaojitolea, sisi sote hutumia Lahajedwali sawa la Google. Baada ya saa mbili, huwa tumemaliza kazi ambayo ingechukua wiki mbili" anasema Kira Lanier, Msimamizi wa Maendeleo katika shirika la Thrive DC. "Iwapo hatujaketi pamoja, tunaweza kuwasiliana kupitia gumzo letu la kikundi kwenye Hangout."

“Kwa kutumia Google Workspace, tunaweza kufanya kazi kwa haraka na kutumia muda mwingi kuhudumia jumuiya.”

Kira Lanier, Msimamizi wa Maendeleo katika shirika la Thrive DC


"Kuhudumia jumuiya" kuna maana ya kipekee kwenye shirika la Thrive DC. Inahusu kutoa misaada ya chakula na huduma kwa makundi ya watu ambao wako katika hatari kubwa ya kuathiriwa kila siku. Pia hubuni mipango ya usaidizi kwa wasio na makazi ili warudi tena katika jamii, wajisimamie na wapate kazi na mwishowe warudi nyumbani. Lengo hili bora linahitaji nyenzo nyingi. Njia ya kawaida ya kuchangisha pesa nje ya mtandao bado ni muhimu katika shirika la Thrive DC, ingawa njia za kuchangisha kupitia barua ya moja kwa moja hazina umaarufu. Kama zana ya mtandaoni, mpango wa Ruzuku za Matangazo umewezesha kupatikana kwa fursa mpya ya kuchangisha. “Wahisani wanatufahamu zaidi kuliko hapo awali, hali hii ni kwa sababu tunaweza kutangaza mtandaoni [bila malipo]. Bila Google, tusingekuwa na nyenzo hizi", alisema Alicia Horton, Mkurugenzi Mtendaji. Njia za Thrive DC za kuchangisha mtandaoni sasa zinaimarika kwa zaidi ya asilimia 10 kila mwaka!

Athari za mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

  • Google Workspace imebadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi shirika la Thrive DC linavyofanya kazi, kusimamia wafanyakazi wa kujitolea, kuwasiliana na hata kukuza vipawa! Kwa mara ya kwanza, timu hiyo ilimwajiri mfanyakazi kwa njia ya mtandao. Kwa kutumia jukwaa la Meet kufanya mikutano ya video na Hifadhi ya Google kushiriki hati, kila mtu anaweza kushirikiana kwa urahisi na kwa wakati mmoja kutoka maeneo tofauti.
  • Google Workspace na Ruzuku za Matangazo bila malipo zinawezesha nafasi 1,000 za miadi ya kuonana na madaktari na vifurushi 40,000 vya ziada vya vyakula kila mwaka kwa wateja wa shirika la Thrive DC.
  • Kupitia Ruzuku za Matangazo:
    • Michango ya mtandaoni imeongezeka kwa asilimia 38 kutoka mwaka 2017 hadi 2018.
    • Tovuti yetu imeweza kuonekana sana kiasi kwamba shirika la Thrive DC hupokea maombi ya kutosha ya wafanyakazi wa kujitolea na halitumii muda tena kuajiri. Hatua hii huokoa siku 40 za kazi kila mwaka na kwa kutumia nyenzo za ziada zilizopo, husaidia shirika la Thrive DC kugharamia nafasi 5,400 za miadi ya kuonana na madaktari kwenye jumuiya.

1Source: U.S. Census Bureau, District of Columbia, Quick Facts, 2017
2Source: United States Interagency Council on Homelessness

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.