Washirikishe wahisani wako ukitumia video na Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Anza kutumia uwezo wa simulizi kuhusu biashara kupitia video ili uweze kufikia hadhira ya kimataifa na utangaze malengo yako zaidi. Pia, warahisishie wahisani kutoa ufadhili ukitumia vipengele vya Uhisani wa YouTube (kwa sasa vinapatikana Marekani).

Manufaa

Jinsi Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida hufanya kazi

Utapata uwezo wa kufikia vipengele hasa vyenye umuhimu kwa mashirika yasiyo ya faida:

  • Kadi za Unganisha Popote hukuruhusu uunganishe wahisani kwenye URL yoyote ya nje
  • Vipengele vya Uhisani wa YouTube vinaweza kukusaidia katika uchangishaji wa pesa na kuwashawishi wahisani
  • Chuo cha Watayarishi hutoa mafunzo yanayolenga mashirika yasiyo ya faida

Gundua jinsi Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida husaidia mashirika kujitangaza, kuwasiliana na wahisani na zaidi.

Zana nyingine za kukusaidia ufikie hadhira yako

Mbali na Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida, bidhaa nyingine zinazotolewa kupitia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida zinaweza pia kukusaidia utangaze shirika lako na uchangishe pesa.

Tuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Baada ya kuthibitisha kuwa shirika lako limetimiza masharti, utaweza kuweka bidhaa za Google zinazotimiza mahitaji yako kikamilifu.

Je, una maswali au ungependa kupata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida?

Baada ya shirika lako lisilo la faida kuthibitishwa na umesajiliwa kwenye Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida, angalia nyenzo zetu na Maswali Yanayoulizwa Sana ili upate manufaa zaidi ya mpango.