Shirikiana, pata tija na ufanye kazi kwa njia bora zaidi kwa kutumia Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida
Lisaidie shirika lako lisilo la faida lishirikiana kwa njia bora zaidi kwa kutumia programu mahiri na salama za biashara kama vile Gmail, Hati, Kalenda, Hifadhi na Google Meet, ili uweze kuangazia mambo muhimu zaidi.
Linganisha mipango kisha uchague toleo la Google Workspace linalofaa zaidi shirika lako lisilo la faida. Weka Gemini ya kutumia katika Google Workspace ili ikusaidie kuandika, kukupa taswira, kupanga, kuwasiliana kwa ukaribu zaidi na mengine mengi.
Manufaa
Jinsi Google Workspace inavyofanya kazi
Workspace huipatia shirika lako lisilo la faida kila kitu unachohitaji ili kufanya jambo lolote, sasa katika sehemu moja. Mipango yote ya Google Workspace hutoa barua pepe maalum ya shirika lako lisilo la faida na inajumuisha zana za kushirikiana kama vile Gmail, Kalenda, Meet, Chat, Hifadhi, Hati, Majedwali, Slaidi, Fomu, Tovuti na zaidi.
Linganisha ofa za mashirika yasiyo ya faida
Kupitia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, masharika ambayo yanatimiza masharti yanapata uwezo wa kufikia ofa za Google Workspace kwa bei zilizopunguzwa
Kila mpango unajumuisha
Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na mapunguzo ya shirika lisilo la faida ya Business Standard na Business Plus yana kikomo cha juu zaidi cha watumiaji 2,000. Hakuna kikomo cha chini au cha juu cha mapunguzo ya mipango ya Enterprise.
Wateja wa Google Workspace huenda wakafikia vipengele vya ziada kwa muda mfupi wa ofa.
Gundua jinsi mpango wa Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida husaidia mashirika kuratibu watu wanaojitolea, kushirikiana katika maeneo yaliyo na majira tofauti ya saa na zaidi.
Girl Scouts of Japan
Shirika la Girl Scouts of Japan hutumia zana za Google kuendeleza mipango, kulinda data yao na kuwawezesha wasichana na wanawake wachanga kote nchini.
Crime Victims Treatment Center
Kwa kutumia Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, Crime Victims Treatment Center huweka maelezo nyeti kwa usalama na yakiwa yamepangwa na pia kurahisisha shughuli.
Nuru International
Google Workspace husaidia shirika la Nuru kufanya shughuli zake za kila siku vizuri zaidi na kwa ufanisi kwenye maeneo 11 yanayotumia saa tofauti za eneo.
Zana nyingine za kukusaidia ushirikiane na uratibu mambo
Mbali na Google Workspace, bidhaa nyingine zinazotolewa kupitia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida zinaweza pia kukusaidia ufanye mambo mengi zaidi kwa pamoja na wengine.
Tuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida
Baada ya kuthibitisha kuwa shirika lako limetimiza masharti, utaweza kuweka bidhaa za Google zinazotimiza mahitaji yako kikamilifu.
Je, una maswali au ungependa kupata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia mpango wa Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida?
Baada ya shirika lako lisilo la faida kuthibitishwa na umesajiliwa katika mpango wa Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, angalia nyenzo zetu na Maswali Yanayoulizwa Sana, ili uweze kupata manufaa zaidi ya Workspace.