Onyesha athari ya shirika lako lisilo la faida ukitumia huduma za Ramani na Google Earth

Tengeneza maonyesho ya data yanayoshawishi ili ufuatilie na ushiriki athari ya shirika lako. Pia, tumia Jukwaa la Ramani za Google ili uwasaidie watu kupata nyenzo na mipango ya jumuiya yako iliyo karibu nao.

Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida hutoa masalio ya Jukwaa la Ramani za Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Manufaa

Jinsi huduma ya Ramani na Google Earth hufanya kazi

Zana za kuchakata na kuonyesha data za Google Earth hutoa aina nyingi ya vipengele vinavyobadilika, kama vile uwezo wa kuwaelekeza wahisani kwenye biashara kupitia onyesho la mtandaoni. Pia, tengeneza onyesho bora na uangazie data ya kushawishi kwenye ramani ukitumia toleo linalolipishwa la Jukwaa la Ramani za Google.

Gundua jinsi huduma ya Ramani na Google Earth huyapa mashirika yasiyo ya faida zana za kufuatilia na kushiriki athari kwa kutumia video za data ya kushawishi.

Zana nyingine za kukusaidia uonyeshe athari ya kazi yako

Mbali na huduma ya Google Earth na Jukwaa la Ramani za Google, bidhaa nyingine zinazotolewa kupitia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida zinaweza pia kukusaidia ushiriki maonyesho ya data ya kazi yako.

Tuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Baada ya kuthibitisha kuwa shirika lako limetimiza masharti, utaweza kuweka bidhaa za Google zinazotimiza mahitaji yako kikamilifu.

Je, una maswali au ungependa kupata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia huduma ya Ramani na Google Earth?

Baada ya shirika lako lisilo la faida kuthibitishwa na umethibitishwa kupata masalio ya Jukwaa la Ramani za Google, angalia nyenzo zetu na Maswali Yanayoulizwa Sana, ili upate manufaa zaidi ya zana.