Hamasisha watu kuhusu dhamira ya shirika lako lisilo la faida, washirikishe wahisani wapya, changisha pesa kwa njia mbalimbali mtandaoni—fanya mambo haya yote na zaidi unapojiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.
-
Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida
Lisaidie shirika lako lisilo la faida lishirikiana kwa njia bora zaidi kwa kutumia programu mahiri na salama za biashara kama vile Gmail, Hati, Kalenda, Hifadhi na Google Meet, ili uweze kuangazia mambo muhimu zaidi.
-
Ruzuku za Matangazo kutoka Google
Vutia wafadhili, tangaza shirika lako na uandikishe watu wanaojitolea ukitumia ufadhili wa matangazo kwenye huduma ya Tafuta na Google.
-
Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida
Anza kutumia uwezo wa simulizi kuhusu biashara kupitia video ili uweze kufikia hadhira ya kimataifa na utangaze malengo yako zaidi. Pia, warahisishie wahisani kutoa ufadhili ukitumia vipengele vya Uhisani wa YouTube (kwa sasa vinapatikana Marekani).
-
Google Earth na Ramani
Tengeneza maonyesho ya data yanayoshawishi ili ufuatilie na ushiriki athari ya shirika lako. Pia, tumia Jukwaa la Ramani za Google ili uwasaidie watu kupata nyenzo na mipango ya jumuiya yako iliyo karibu nao.
Hatua za kupata bidhaa za Google
Thibitisha kwamba umetimiza masharti ya kujiunga
Tuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida
Shirika lako lisilo la faida litakapothibitishwa, tutakujulisha kupitia barua pepe
Kisha unaweza kuweka na kutumia bidhaa mahususi
Tuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida
Baada ya kuthibitisha kuwa shirika lako limetimiza masharti, utaweza kuweka bidhaa za Google zinazotimiza mahitaji yako kikamilifu.