WaterAid

WaterAid hubadilisha maisha ya watu maskini na watu waliotengwa zaidi kwa kuboresha uwezo wa kupata maji safi, vyoo salama na mipango ya usafi.

Kiasi cha Utendaji

Kubwa

Sekta

Kimataifa, Masuala ya Kimataifa

Malengo

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

WaterAid

Tovuti

https://www.wateraidamerica.org/

Changamoto

Mawasiliano jumuishi ya mfululizo ni muhimu zaidi katika kuunganisha kikundi cha wafanyakazi wenye bidii na waliojitolea katika WaterAid. Ili kumaliza tatizo la maji na usafi, ni lazima WaterAid iendeleze uhamasishaji ili ibaki kuwa shirika linalopewa kipaumbele zaidi na wahisani wa sasa, huku likiendelea kuwavutia wafadhali watarajiwa.

Hadithi

WaterAid hutumia YouTube kuunganishwa na hadhira kwa njia nyingi. Maudhui ya kuchangamsha na yenye ucheshi yanayovuma mtandaoni huvutia hadhira ya watu wenye umri mdogo na video kutoka kwenye ofisi za nyanjani huangazia mipango ya kimataifa.

Hifadhi ya Google ni kipengee kingine muhimu zaidi ambacho huwaruhusu wafanyakazi wafikie faili muhimu zaidi kwenye kifaa au mahali popote walipo. Hatua hii ni muhimu hasa wakati wa kuwasiliana na ofisi 38 katika mabara sita.

WaterAid hutumia pia Google Analytics pamoja na Kidhibiti Lebo cha Google kuboresha uwezo wa kufuatilia, kama vile kutambua watu wanaotembelea tovuti kulingana na mtumiaji, si tu kulingana na kifaa. Hatua hii hutoa njia dhahiri zaidi ya kuelewa jinsi watu wanavyoshawishika kwenye tovuti ya WaterAid.

“Hatua ya kuyapa mashirika ya uhisani uwezo wa kiwango cha kibiashara wa kufikia zana za Google, huyapa mashirika yasiyo ya faida mfumo kamili jumuishi ili kuandika, kulenga, kutangaza na kufuatilia ujumbe kwa hadhira zao za msingi huku ikiyaruhusu kushindana kupitia nyenzo nyingi za mashirika na biashara kubwa za bidhaa za watumiaji.”

Tiffany Langston, Msimamizi wa Mawasiliano, WaterAid

Athari

Zana zinazopatikana kupitia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida zimeiruhusu WaterAid kubuni maudhui ya mtandaoni ambayo yanavutia na kushirikisha zaidi, hatua ambayo imesababisha kuunganishwa zaidi na wafadhili wapya. Kwa kuelewa hadhira yake mtandaoni, WaterAid imeweza pia kuboresha tovuti yake ili kutoa hali bora zaidi ya utumiaji. Kupitia ufadhili huu wote, WaterAid ilifanikiwa kufikisha maji safi kwa watu milioni mbili na kutoa huduma za usafi kwa watu milioni tatu mwaka uliopita.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.