Kiasi cha Utendaji
Wastani
Sekta
Sanaa, Utamaduni na Masomo ya Kibinadamu
Malengo
Hamasisha
Hifadhi na upange vipengee kwenye wingu
Kushiriki maelezo
Malengo Kushirikisha hadhira
Ongeza idadi ya wanaofuatilia
Panua hadhira yako
Pata watu wanaofuatilia shirika lako
Tathmini utendaji wa tovuti yako
Tengeneza Maudhui ya YouTube
Vutia watu wanaotembelea tovuti yako
Wasiliana na ushirikiane kwa njia bora zaidi
Aliyepiga Picha
Makavazi ya Van Gogh: picha ilipigwa na Jan Kees Steenman
Changamoto
Miaka kumi iliyopita, Makavazi ya Van Gogh yaliajiri Msimamizi wa kwanza wa Maudhui Dijitali. Leo, idara ya Mawasiliano ya Kidijitali ina watu sita wenye lengo la kuwasiliana na hadhira ya kimataifa, kuuza tiketi za kuingia katika makavazi, kuhamasisha kuhusu matukio maalum na kuelimisha watu duniani kuhusu maisha na sanaa kwenye Vincent van Gogh. Timu kubwa huwa na changamoto kuhusu kushirikiana kwa njia bora lakini hutoa nyenzo zaidi za kushughulikia fursa kubwa. Mfano moja ni kusambaza habari kuhusu The Mesdag Collection, ambayo ni makavazi inayopatikana Hague inayosimamiwa na Makavazi ya Van Gogh. The Mesdag Collection haijulikani sana ikilinganishwa na Makavazi ya Van Gogh na bado haina jina la biashara wala wateja wengi. Ili kufanya ifahamike zaidi na kuongeza idadi ya wateja, Idara ya Dijitali imeanza kutumia zana za Google.
Simulizi
Makavazi ya Van Gogh yanayopatikana Amsterdam, yaliyofunguliwa mwaka wa 1973, hufanya shughuli za maisha na kazi ya Vincent van Gogh na sanaa ya wakati huo itambuliwe na watu wengi zaidi iwezekanavyo ili wafahamu na kufurahia. Idadi ya mikusanyiko ya Van Gogh iliyo katika makavazi haya ndiyo ya juu zaidi duniani. Mikusanyiko hii ni ya michoro na picha zilizopakwa rangi na Van Gogh. Katika mwaka wa 2016, makavazi hayo yalipokea wageni milioni 2.1 na yalikuwa ya pili kutembelewa zaidi nchini Uholanzi. Vile vile, Mesdag Collection inayopatikana Hague ni makavazi yaliyoundwa na msanii na mkusanyaji Hendrik Willem Mesdag na mkewe Sientje Mesdag. Sasa inasimamiwa na Makavazi ya Van Gogh. Makavazi hayo (na makazi ya awali ya Hendrik na Sientje Mesdag) huonyesha mikusanyiko ya sanaa za Mesdags: Picha zilizopakwa rangi na wasanii kutoka French Barbizon School na Dutch Hague School.
Makavazi hayo hutumia Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kushirikiana vyema ndani ya shirika na makavazi mengine. Hutumia Google Meet kuwasiliana wakati ambapo ni vigumu kupanga mkutano wa ana kwa ana. Shughuli ya kushirikiana na kushiriki faili ni rahisi zaidi kupitia Hati na Hifadhi ya Google. Hamna haja ya hati zilizofungwa au matoleo ya kawaida ukiwa na Hati za Google. Kila mtu anaweza kuona na kubadilisha hati moja kwa wakati mmoja. Kwa usimamizi wa vipengee, Makavazi ya Van Gogh hutegemea kimsingi Hifadhi ya Google.
Ruzuku za Google Ad hutumiwa kuhamasisha si tu kwenye Van Gogh Museum, bali pia katika The Mesdag Collection. Zilitoa matangazo ya maandishi yanayolenga mahali ambayo yamesaidia kuhamasisha watu kuhusu Van Gogh Museum huku yakiimarisha mauzo ya tiketi. Timu ya Mawasiliano ya Kidijitali ilitumia Google Analytics ili kupima athari ya moja kwa moja ya matangazo katika mauzo ya tiketi na ikapata kuwa Ruzuku za Google Ad huchangia asilimia 15 ya jumla ya mauzo ya tiketi kwenye Van Gogh Museum na huvutia asilimia 40 ya jumla ya wanaotembelea tovuti.
"Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida hutusaidia kufanya sanaa ya Vincent van Gogh iwafikie watu wengi zaidi duniani kuliko hapo awali. Zaidi ya hayo, zana za kuchapisha, kusambaza na kutangaza maudhui na kufuatilia matokeo, yote huchangia katika dhamira ya makavazi."
Edith Schreurs, Makavazi ya Van Gogh
Athari
Kutokana na Ruzuku za Google Ad, idadi ya wanaotembelea tovuti ya Mesdag Collection imeongezeka mara mbili. Bila shaka, Google Ads huelekeza asilimia 44 ya jumla ya wanaotembelea tovuti ya Mesdag Collection na ndicho chanzo cha watazamaji kinachoongoza kwa jumla. Katika Makavazi ya Van Gogh, matokeo halisi ya Google ndicho chanzo kinachoongoza cha watazamaji na huelekeza asilimia 39 ya watazamaji. Matumizi ya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida yamekuwa na athari kubwa kwenye shirika na jumuiya yetu.
Zaidi ya hayo, saa za kazi za makavazi hutofautiana kulingana na misimu, kwa hivyo timu ya Dijitali pia husasisha ukurasa katika huduma ya Google Business Profile ili iwe rahisi kwao kupanga kutembelewa. Zaidi ya hayo, timu ya Maudhui ya Kidijitali iligundua umuhimu wa Google Analytics na hukagua akaunti yake ya Google Analytics kila siku ili kuelewa mitindo ya watumiaji wa mtandao na mahali wanakotoka. Kituo cha YouTube kimeimarika na sasa kina zaidi ya watu 4,039 wanaokifuatilia na Makavazi ya Van Gogh hutengeneza maudhui halisi ya YouTube kama vile video zilizoangaziwa ‘Meet Vincent’ (tayari imetazamwa mara 27,156) na vionjo vya maonyesho, ili kuendeleza dhamira yake ya kuelimisha ulimwengu kuhusu Vincent van Gogh.
Watu wengi wana hamu ya kufahamu kuhusu vipengele vya sanaa na shughuli za maisha ya Vincent van Gogh. Kazi zake za sanaa huvutia macho na ni muhimu kwa makavazi kutoa mchanganyiko mzuri wa video bora kuhusu Vincent van Gogh (za kuelimisha, mada za utafiti, vionjo vya maonyesho, n.k.). Kadri maudhui ya video yanavyozidi kuwa muhimu, timu ya Mawasiliano ya Kidijitali imewekeza nyenzo ili kutengeneza maudhui bora ya video ili kushiriki na watazamaji duniani kote. Utengenezaji wa video za makavazi hufanywa kwa ushirikiano kati ya idara kadhaa (timu za Mawasiliano ya Kidijitali, Elimu na Ukalimani, Utangazaji) ili kuleta uwiano bora kati ya maudhui ya kina na hatua muhimu za kuchukuliwa. Katika miaka ya hivi majuzi YouTube imekuwa mtambo muhimu wa kutafuta na makavazi huonyesha umakini katika uboreshaji wa video kwa ajili ya mtambo wa kutafuta na huhakikisha kupachika video kwenye mifumo tofauti kama vile kwenye tovuti yake.