Kiva

Dhamira ya Kiva ni kupanua uwezo wa kupata fedha ili kusaidia kustawi kwa jamii ambazo hazipati huduma ya kutosha. Kwa kutumia intaneti na mtandao wa mashirika madogo ya kutoa fedha duniani kote, Kiva huwaruhusu watu wakopeshe kuanzia $25 ili kusaidia kubini fursa kote duniani.

Kiasi cha Utendaji

Kubwa

Sekta

Umma, Manufaa ya Jamii

Malengo

Changisha pesa

Hamasisha

Pata wafadhili

Tengeneza Maudhui ya YouTube

Bidhaa

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Kiva

Tovuti

https://www.kiva.org/

Changamoto

Kiva hufanya mashirika madogo ya kutoa fedha kwa kuunganisha wakopeshaji na wakopaji kote duniani. Mara nyingi, wakopaji hawa hawana uwezo wa kupata mtaji wa kukuza biashara zao, kutimiza mahitaji ya matibabu au elimu kwa familia zao au kuboresha hali zao za maisha kwa jumla. Ili Kiva iweze kuwaunganisha wakopaji na wakopeshaji, inahitaji kukuza shirika na kufahamisha watu kuhusu kazi yao muhimu.

Hadithi

Kiva ilianza kutumia huduma ya Ruzuku za Matangazo ili kutangaza shirika lake. Kwa sasa ni chanzo kikuu cha watu wanaotembelea tovuti yao mtandaoni. Mkopeshaji mtarajiwa anapofanya utafiti kuhusu jinsi anavyoweza kukopesha pesa kwa mashirika madogo, Kiva inaweza kutayarisha maelezo ya wateja waliotimiza mahitaji ya kukopa. Kiva inaweza kupata watu ambao tayari wamevutiwa na dhamira yao na ambao tayari wanatafuta kujiunga na mashirika ya kukopesha.

Kiva pia imetumia YouTube ili kuwezesha jumuiya yake kwa kuhimiza mashirika mengine, wafanyakazi wa kujitolea na jumuiya yake ya watumiaji, watayarishe na kupakia video za YouTube kila siku.

“Kufikia sasa, Kiva imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1.3 za Marekani kwa wateja milioni 3.3, wakiwemo wakulima, wajasiriamali, familia na watu wengine wasio na akaunti za benki kote duniani. YouTube na Ruzuku za Matangazo kutoka Google ni sehemu muhimu ya mikakati ya utangazaji wa Kiva. Uonekanaji wa shirika unaofanywa na zana hizi umesaidia zaidi katika kudumisha athari ya Kiva.”

Tracey Gill Miller, Msimamizi wa Utangazaji Kulingana na Hatua za Wateja, Kiva

Athari

Jacqueline alilazimika kutoroka nyumbani kwake nchini Burundi na kuanza maisha mapya nchini Rwanda. Mwanzo, alitatizika kupata chakula na kutimiza mahitaji ya watoto wake watatu. Lakini Jacqueline ana bidii, mkweli na mjasiriamali. Alianzisha biashara ya kutengeneza sabuni kupitia msaada wa mkopo wa Kiva na kubadilisha maisha yake.

Wakopeshaji 213 kote duniani walichangia kumkopesha Jacqueline $5,925 ili anunue malighafi na mashine ndogo ya kutengeneza sabuni.

Kufikia sasa, Jacqueline amewaajiri watu kadhaa kwenye biashara yake inayoimarika na anaweza kuwalipia watoto wake karo ya shule. Anawashukuru wakopeshaji wa Kiva na anajitahidi “kuendeleza mtindo kama huo wa kutoa misaada kwa watu wengine wenye mahitaji.”

Idadi ya watu wanaotembelea tovuti inayotokana na huduma ya Ruzuku za Matangazo, michango inayoonekana kwenye Ramani za Google na matendo ya jumuiya kupitia YouTube, yamesaidia Kiva kufikia lengo lake na kutimiza dhamira yake wa kutoa uwezo wa kupata fedha ili kusaidia kustawi kwa jamii ambazo hazipati huduma ya kutosha.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.