Girl Scouts of Japan

Madhumuni ya shirika la Girl Scouts of Japan ni kuwawezesha wasichana na wanawake wachanga kuwaza na kufanya kazi wenyewe kwa furaha na usalama wao wakiwa wananchi wanaowajibika.

Kiasi cha Utendaji

Ndogo

Sekta

Huduma za Jamii

Malengo

Shirikiana kwa ufanisi zaidi

Wasiliana na wahisani

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

ⒸGirl Scouts of Japan

Tovuti

https://www.girlscout.or.jp/

Changamoto

Girl Scouts of Japan ni shirika la kitaifa, linalojumuisha Mabaraza 47 ya Mitaa na takribani wanachama 40,000. Ni mwanachama wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts ambalo ni Vuguvugu kubwa zaidi la kujitolea linalozingatia masilahi ya wasichana na wanawake wachanga. Shirika la Girl Scouts huwasaidia na kuwawezesha wasichana na wanawake wachanga kukuza uwezo wao kikamilifu kupitia elimu isiyo rasmi.

Kama shirika la kitaifa, Girl Scouts of Japan lilikuwa na changamoto ya mawasiliano kati ya wanachama wote. Kwa kuwa lina vikundi vingi na wanachama wa umri tofauti, walihitaji mfumo wa biashara ulio salama na bora ili kuhakikisha vikundi vyote vimepangwa na kuwa taarifa binafsi kuhusu watoto imewekwa salama. Kama shirika kuu la mabaraza ya mitaa, faili zao huwa na taarifa binafsi kuhusu wasichana na wanawake wachanga katika kila kundi na baraza, pamoja na watu wazima ambao huwawakilisha kama Viongozi wao. Kwa kuwa lina matawi kote nchini, ufuatiliaji na ukaguzi wa ufanisi wa shughuli ni muhimu. Viongozi wa Makundi na mabaraza ya mitaa huripoti kwa shirika la Girl Scouts of Japan kuhusu mahudhurio, urudiaji wa matukio na vipimo vingine vya athari ili kuhakikisha kuwa shirika lao linatoa huduma bora iwezekanavyo. Kutokana na nyenzo chache, lilihitaji njia ambayo ingetumiwa kwa urahisi nchini kote katika matawi mbalimbali ya mabaraza ya mitaa.

Simulizi

Kupitia “Moyo wa Girl Scouts” wa kujaribu kitu kipya bila kuogopa, shirika la Girl Scouts of Japan limejumuisha kundi la bidhaa za mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ili kutekeleza utendaji bora kote kwenye makundi na mabaraza mengi ya mitaa. Kwanza, walianza kutumia Google Workspace ili kupanga shughuli za biashara kwenye mabaraza yao ya mitaa. Kwa kupachika fomu kwenye tovuti yao, wanaweza kutoa mipango ya masomo ya mtandaoni kupitia Fomu za Google kwa wanachama wa Girl Scout. Mpango wa masomo ya mtandaoni umewapa wanachama wengi fursa ya kupata ujuzi kuhusu Girl Scouting na ujuzi wa kukuza Uongozi. Ingawa mpango wa Girl Scout umekuwepo kwa zaidi ya karne moja, shirika la Girl Scouts of Japan limeboresha kazi zake kwa kutumia mijarabu kupitia Fomu ya Google ili kuwasaidia wasichana na wanawake wachanga kuboresha maarifa na ujuzi wao, huku wakipata beji kutoka mabaraza ya mitaa kote nchini.

Wafanyikazi katika shirika la Girl Scouts of Japan wana viwango tofauti vya maarifa ya kiufundi, na bidhaa kama Fomu na Majedwali ya Google huwaruhusu kushiriki habari na kupata muhtasari wa data bila kuweka wenyewe. Kwa kuwa ni shirika kuu la mabaraza ya mitaa, Google Workspace huwaruhusu kushiriki tu hati na watumiaji ambao wana idhini ya kufikia katika kila tawi, hali inayoboresha hatua za faragha. Kwa kuwa faili sasa zinaweza kushirikiwa kwenye mabaraza ya mitaa, kila kundi linaweza kushiriki mbinu bora, shughuli za kukuza timu, na shughuli nyingine ili kuendeleza kazi zao. Wakitumia Gmail, matatizo yao ya awali kuhusu barua taka, programu hasidi na matatizo mengine ya usalama yamepungua kupitia mipangilio ya faragha ya Google. Kwa kuweka huduma ya Tovuti za Google, mabaraza ya mitaa na wanachama mbalimbali wanaweza kufikia maelezo yanayofaa kama vile mafunzo kwa Viongozi wa Vikundi na vijitabu vya maelezo. Hatua hii inaruhusu kushirikiwa haraka kwa maelezo na taarifa katika wakati halisi kwenye mabaraza ya mitaa na wanachama wanaosaidiwa na shirika la Girl Scouts of Japan.

Si bidhaa kutoka mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ambazo zimesababisha uboreshaji wa shughuli za ndani za biashara, lakini hivi majuzi shirika la Girl Scouts Japan lilitumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kutekeleza mawasiliano na shughuli za nje. Kwa kutumia Ruzuku za Matangazo na YouTube wanakuza uwepo mtandaoni ili kupata wanachama wapya na kushiriki kazi njema na matukio yanayofanyika katika kila eneo. Video zao kwenye YouTube husaidia kuonyesha kazi wanayoifanya ili kuwawezesha wasichana na wanawake wachanga ikiwa ni pamoja na shughuli za kukuza timu, kuimba kwa pamoja, na kambi za msimu wa jua.

Ili kushiriki maelezo na kuongeza idadi ya watu wanaohudhuria matukio yao, wao hutumia Ramani za Google kuwasaidia wasio wanachama wanaovutiwa katika Girl Scouting kupata kwa urahisi matukio yanayofanyika kote Japani. Pia wanatumia API za Ramani za Google kupitia mpango wa Earth Outreach ili kutoa mtazamo wa jumla kuhusu athari zao kwa wanachama wa sasa, na pia watu wanaoweza kujiunga. Kwa kuunganisha API ya Ramani za Google na YouTube, walianzisha Onyesho la Mtandaoni la vituo vitano vya Girl Scout duniani kote. Hatua hii inahimiza mtazamo wa jumla, na hufanya wanachama wake kujihisi sehemu ya jumuiya kubwa duniani kote.

Zana za mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida hazisaidii tu katika ufanisi na ubora wa mipango ya shirika la Girl Scouts of Japan, lakini pia husaidia kuonyesha kazi yao muhimu ili kuwahimiza na kuwawezesha wasichana na wanawake wachanga.

Rumiko Meguro, GSJ ofisi kuu, Timu ya Mahusiano na Uchangishaji

Athari

Kama shirika kubwa la kitaifa, jitihada zaidi zimeleta ufanisi. Mpango wao wa masomo ya mtandaoni - maudhui yanayobainishwa na Fomu ya Google - uliwaruhusu zaidi ya wanachama 7,000 kupewa mafunzo kuhusu chochote kuanzia maarifa kuhusu Girl Scouting na ujuzi wa maisha. Kwa mtazamo wa kifedha, Google Workspace imetoa mifumo ya ubora wa juu zaidi ya usalama ambayo inaweza kutekelezwa katika maeneo mengi.

Hatua ya kutumia Google Workspace imeboresha zaidi ufanisi wa shughuli zao. Awali, baadhi tu ya wafanyikazi ndio walitumia bidhaa za Google kwa kiasi fulani, lakini bado Google Workspace haikuwa imesakinishwa kwenye shirika. Kwa hivyo, iliwabidi kuweka akaunti nyingi za barua pepe, hali ambayo ingesababisha hatari ya kiusalama. Shirika lilipoanza kutumia Google Workspace, kila mfanyakazi alipata akaunti moja tu ya kufanya shughuli zote ambayo angeweza kuifikia mahali popote - hatua ambayo iliondoa hatari ya kupoteza hati za wafanyakazi iwapo angeondoka. Google Workspace huwaruhusu kusimamia watumiaji wao ndani ya shirika, kutoa taarifa kwa wafanyikazi wao wengi katika shirika kwa haraka na kwa ufanisi. Awali, mfanyakazi anayesimamia maelezo ya shirika na mfumo wa teknolojia ya mawasiliano alihitaji kutuma maombi ya kubadilisha akaunti, kama vile kuweka wanachama wapya au kufuta akaunti ya wafanyakazi waliostaafu, kwa kumuuliza mtoa huduma wa nje kupitia lahajedwali. Hatua hii inawaruhusu kutumia muda mchache kufanya shughuli za msingi za shirika lao, na kutumia muda mwingi zaidi katika juhudi zao za maendeleo ili kuwafikia wasichana na wanawake wengi wachanga na kuendelea na kazi za mpango wao.

Zana za mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida pia iliimarisha kuonekana kwa shirika lao na juhudi zao za kusaidia wasichana na wanawake wachanga na kuwakuza. Awali, matukio yao yaliorodheshwa kwenye ukurasa katika tovuti - ikionyesha matukio mengi katika orodha ndefu ambayo waliohudhuria walihitaji kupitia. Kwa kutumia Ramani za Google waliweza kupachika ramani kwenye tovuti yao na kuweka matukio katika muda halisi. Kila tukio limewekewa rangi, kulingana na mwezi au mada (kama vile “Siku ya Girl Scouts”) ili kuwasaidia watu wanaovutiwa na Girl Scouting kupata matukio yaliyo karibu kwa haraka ili kuhudhuria. Kwa kujumuisha matukio kwenye Ramani za Google na kuonyesha eneo husika, wameongeza idadi ya wanaohudhuria na maelezo ya tukio yametazamwa zaidi ya mara 18,000. Wanaotaka kujiunga hawahitaji tena kutafuta ili kupata mkutano ulio karibu, lakini wanaweza kufungua tu ramani na kupata fursa ya kuwasiliana na wengine.

Hatua ya kushiriki kazi muhimu wanayofanya na kuonyesha athari zake kwa wasichana na wanawake wachanga ni muhimu kwa ufanisi wa shirika la Girl Scouts of Japan. Mpango wa Ruzuku za Matangazo umeboresha uwepo wao mtandaoni, hali iliyofanya zaidi ya wageni 3,000 kutembelea tovuti yao kila mwezi. Hii imesababisha ongezeko la asilimia 500 la wageni katika miezi miwili tu. Kwa kampeni za ulimwengu kama vile “Komesha Unyanyasaji” walitunga matangazo yanayohimiza usawa wa jinsia na ulinzi dhidi ya unyanyasaji ili kuhamasisha na kuongeza kuangaziwa kwa kampeni hii kwenye vyombo vya habari Japani. Vilevile, kituo chao cha YouTube huangazia orodha ya kucheza ya Girl Scout wakicheza wimbo “I’ll Think of You” - uliotungwa na Kurt Schneider, kama shughuli ya kukuza timu. Makundi na mabaraza mengi ya mitaa yalitoa video - ina michango 43 kufikia sasa. Hii hutumika kuonyesha mifano ya shughuli ambazo Girl Scout wanaweza kufanya, vilevile kuwaelekeza wanaotaka kujiunga kwenda kwenye tovuti kupitia kadi na vidokezo. Ikiwa imetazamwa zaidi ya mara 20,000 katika baadhi ya video, YouTube imetumika kuonyesha kazi wanazofanya ili kuwasaidia na kuwawezesha wasichana na wanawake wachanga.

Shirika la Girl Scouts of Japan lina mipango mingi - kuanzia mpango wa 'kukuza hadhi' uliobuniwa kwa usaidizi wa WAGGGS na DOVE, hadi kwa kampeni ya Kukomesha Unyanyasaji ili kusaidia kupunguza matukio ya unyanyasaji dhidi ya wanawake, na kambi na matukio mbalimbali kote nchini. Zana za mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida hazisaidii tu katika kupanga na kuboresha mipango hii, lakini pia husaidia kuonyesha kazi yao muhimu ili kuwahimiza na kuwawezesha wasichana na wanawake wachanga.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.