Sekta
Wanyama na Mazingira
Malengo
Changisha pesa
Hamasisha
Onyesha data kwenye ramani
Aliyepiga Picha
NRDC, Point Loma, Kip Evans
Changamoto
NRDC inaelewa umuhimu wa simulizi kuhusu biashara linapoelimisha umma na kuhimiza usaidizi wa sera ya mazingira. Ili kulinda dunia, kama mojawapo wa mashirika makubwa na yenye ushawishi katika utetezi wa mazingira, Natural Resources Defense Council inahitaji kuwasiliana vizuri, kuelewa data inayokusanya na kuelekeza watu wengi kwenye tovuti yake.
Hadithi
Kwa kuonyesha data na kuelekeza watu kwenye tovuti yake, NRDC inaweza kuhamasisha watu kuhusu masuala ya mazingira ambayo yanatuathiri sote. NRDC inapotaka kusimulia hadithi yake, zana za Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida huisaidia katika kila hatua.
Natural Resources Defense Council hutumia Ramani za Google na Google Earth kukuza uwezo wa utetezi kwa kuonyesha masuala yao ya mazingira kwa njia thabiti na inayoeleweka.
Pia, NRDC hutumia G Suite kueneza ujumbe wa shirika hilo, Google Analytics huwasaidia kubainisha athari za ujumbe wao. Mfumo wa YouTube umewasaidia kupata picha na video kuhusu masuala makuu ya mazingira. Pia wanatumia Ruzuku za Google Ad kuhakikisha kuwa wanaboresha uonekanaji kutokana na matendo wanayofanya.
“Katika wiki za kwanza za janga la mafuta ya Ghuba, NRDC ilitumia kituo cha YouTube [kuonyesha] picha zinazoshawishi … Mojawapo ya video tulizochapisha, ‘Yours Truly, BP,’ ilitazamwa zaidi ya mara 100,000 bila kulipia kuitangaza.”
Kim Ranney, Mkurugenzi wa Utangazaji wa Biashara kwa Kutumia Maudhui ya Kuvutia, NRDC
Athari
Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida umefaa zaidi NRDC katika utumaji wa ujumbe wao kwa hadhira iliyopo na mpya. Google Ads imeelekeza zaidi ya watu milioni 7.7 kwenye tovuti yao na bado inaendelea kuelekeza. Hali hii inalingana na dola milioni 5.3 katika thamani ya matangazo.
Kupitia masimulizi ya kushawishi ya video, NRDC inalenga kuelimisha, kuhamasisha na kushirikisha hadhira mpya; inatumia kituo cha YouTube kuwafikia watu wengi iwezekanavyo. Baada ya Kumwagika kwa Mafuta Ghuba, video inayoangazia picha za watu na wanyama walioathiriwa na janga hilo ilitazamwa zaidi ya mara 100,000 bila kulipia kuitangaza.