Charity: Water
Watu milioni 663 duniani wanaishi bila maji safi. Katika Charity: Water, dhamira yetu ni kubadilisha hali hiyo kwa kuleta maji safi na salama ya kunywa kwa watu katika nchi zinazoendelea. Shirika linafanya kazi na washirika wake katika nchi za kigeni na limekamilisha zaidi ya miradi 21,000 ya maji na kufanya zaidi ya watu milioni 6.4 waweze kupata maji, huduma za usafi wa mwili na kudumisha mazingira safi.
Dhamira yetu ni kuleta maji safi na salama ya kunywa kwa kila mtu duniani na kwa usaidizi wa Google, tunakaribia kufanikiwa kila siku.
Tyler Riewer, kiongozi wa maudhui ya kibiashara
Athari
“Katika mwaka mmoja, mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ulisaidia kupata ongezeko la asilimia 350 la watu waliotembelea tovuti, ongezeko la asilimia 300 la jumla ya watu waliotembelea tovuti na ongezeko la asilimia 333 kwa waliotazama video.” alisema Tyler Riewer, kiongozi wa maudhui ya kibiashara, Charity: Water
Tangu timu ianze kutumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, shughuli zao za mtandaoni zimeimarika kwa haraka. Shirika pia lilibuni jumuiya ya wahisani wenye ari kupitia video za YouTube zilizotoa ujumbe wa shukrani kwa watu mahususi, uwezo wa Ramani za Google na pia kupitia matangazo yanayotegemea utafutaji na mitandao jamii.
Na katika mwaka wa 2015, Charity: Water ulizindua kampeni yake ya kila mwaka ya kuchangisha mnamo Septemba. Ilikuwa na mada #NothingIsCrazy, ambayo iliwahimiza watu wajitolee kwa njia isiyo ya kawaida katika kuchanga pesa za kuleta maji safi. Kupitia usaidizi wa zana za Google, kampeni ilihamasisha karibu wachangishaji binafsi 1,900 na wakachanga dola milioni 1.8, ambazo zilileta maji safi kwa zaidi ya watu 60,000 katika nchi zinazoendelea. Google Analytics ilisaidia timu kuelewa washiriki, kubainisha asilimia ya walioshawishika na chati ya iliyoonyesha mara ambazo video ya tangazo la kampeni ilitazamwa.
Kwa sasa, Charity: Water inatumia uwezo wa kushawishi wa zana za Google kufikia hadhira mpya na kuwahimiza kuwekeza katika mazingira ambako kila mtu ana maji safi kwa kujiunga na mpango wa kuchangisha wa kila mwezi wa shirika hilo, The Spring.
Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.
WaterAid
WaterAid hutumia zana za Google ili kubuni maudhui yanayovutia na kushirikisha zaidi, hali inayosababisha kuunganishwa zaidi na wafadhili.
Jane Goodall Institute
JGI hutumia zana za Google Earth ili kurekodi, kuchanganua na kushiriki maelezo kuhusu uharibifu wa misitu ulimwenguni.
Kiva
Kiva hutumia YouTube ili kuwezesha jumuiya yake kwa kuwahimiza mashirika, wafanyakazi wa kujitolea na watumiaji kushiriki hadithi zao.