Action Against Hunger

Kwa zaidi ya miaka 40, tumejitahidi kupambana na janga la njaa katika takribani nchi 50 duniani kote. Tunaokoa maisha ya watoto na kushirikiana na jumuiya zao kabla na baada ya janga. Tunawawezesha watu watimize mahitaji yao, waone watoto wao wakiwa na afya bora na kudumisha jumuiya zinazostawi. Tunatafuta mara kwa mara suluhu bora, tunaposhiriki maarifa na ujuzi wetu na watu duniani kote. Tunahimiza mabadiliko ya muda mrefu. Hatutakata tamaa hadi tuangamize janga la njaa duniani.

Kiasi cha Utendaji

Kubwa

Sekta

Kimataifa, Masuala ya Nchi za Kigeni

Malengo

Shirikiana kwa ufanisi zaidi

Shiriki hadithi yako

Fikia wafadhili kwa urahisi zaidi

Wasiliana na wahisani

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Jana Asenbrennerova

Tovuti

https://www.actionagainsthunger.org

Changamoto

Utapiamlo hatari sana husababisha vifo vya watoto milioni moja kila mwaka1. Lakini janga hili linaweza kuzuiwa na kutibiwa. Shirika la Action Against Hunger hujitahidi kufikia watoto walio na lishe duni kwa wakati ili kuwaokoa. Kwa bahati mbaya, shirika la Action Against Hunger hupokea ufadhili mdogo wa kusaidia katika utangazaji, mawasiliano na teknolojia ya habari. Ingawa wangependa kuwekeza katika maeneo haya, hawana nyenzo zinazohitajika kukuza mipango yao.

Kama shirika la kimataifa, mawasiliano ni muhimu. Hata hivyo, utumiaji wa zana za mawasiliano zilizo kila mahali za shirika la Action Against Hunger ulikuwa na changamoto. Timu tofauti zilitumia mbinu tofauti za kuwasiliana na kila mara mtu alipotaka kuzungumza na mwenzake, alihitaji kwanza kufahamu jina maalum la mtumiaji kisha kumwongeza kwenye programu husika ya kutuma ujumbe.

Kazi za kuokoa maisha katika shirika la Action Against Hunger zinahitaji kutekelezwa mchana na usiku. Hata hivyo, walitatizika kudumisha seva zao kila wakati. Pamoja na vitisho vya majanga ya kiasili kama vile Kimbuga cha Sandy New York ambacho kingeweza kukatiza nishati ya seva, walikuwa katika hatari ya kupoteza kila kitu.

Kwa kutumia zana za Google, shirika la Action Against Hunger liliweza kukabili changamoto hizi na kuangazia huduma za kuokoa maisha.

Hadithi

Shirika la Action Against Hunger hutegemea mtazamo mpana wa kushughulikia utapiamlo uitwao Usimamizi wa Jamii Kukabili Utapiamlo Hatari (CMAM). Mzazi anaweza kuleta nyumbani lahamu iliyo na madini mengi, protini na karanga yenye kalori nyingi kutibu mtoto wake. Vyakula hivi vya matibabu vilivyo tayari kwa matumizi (RUTF) vinafanana na pande za protini na hazihitaji kutayarishwa au kuhifadhiwa kwenye friji. Kuwatibu watoto nyumbani huondoa haja ya kusafiri mbali kwenda kwenye vituo vya afya, kwa hivyo wazazi wanaweza kuhakikisha kuwa wanafamilia wote wana afya njema.

Ili kusaidia kupambana na utapiamlo, shirika la Action Against Hunger hutumia zana za Google. Ruzuku za Google Ad na YouTube husaidia Action Against Hunger kuchangisha pesa zaidi ili kutekeleza mipango na kupanua hadhira wanayohudumia.

Action Against Hunger hutumia Ruzuku za Google Ad kama sehemu ya mpango wao wa hatua ya dharura janga linapotokea. Kwa mfano, njaa ilipotangazwa Sudan Kusini, walizindua matangazo kwa haraka ya kulenga hoja husika za utafutaji na kuwawezesha watu wachukue hatua za kuokoa maisha. Ebola ilipogonga vichwa vya habari, Action Against Hunger ililenga mara moja maneno muhimu kwa kutumia akaunti yao ya Ruzuku za Google Ad ili kuwashawishi watu wanaotafuta taarifa kuwa watu wanaochukua hatua. Kisha shirika lilitumia Google Analytics kufanya uamuzi unaotokana na data kuboresha uchangishaji na kuimarisha ushiriki wa watumiaji. Kwa kweli, walikaribia kuchangisha maradufu ya mapato ya kila mwaka, kutokana na Ruzuku za Google Ad, na wanatabiri kuwa watafanya hivyo tena mwaka huu.

Tangu shirika la Action Against Hunger lilipoanza kutumia Google Workspace mwaka 2013, mbinu zake za mawasiliano na kushirikiana zimebadilika kabisa. Kwa mfano, Google Meet imekuwa programu yao ya kipekee ya kutuma ujumbe kwenye shirika na kutoa njia ya haraka kwa kila mtu kuwasiliana kwenye mtandao wao wa kimataifa. Sasa mtu aliye kwenye ofisi ya London anaweza kuzungumza kwa haraka na mwenzake aliye New York, kupitia ujumbe wa papo hapo au kwa kuingia kwenye Google Meet (simu ya mkutano wa video). Gmail na Hifadhi ya Google vimekuwa vipengele muhimu vya kuongeza tija. Sasa Google Workspace imekuwa uti wa mgongo wa shirika lao, hali inayowasaidia kupata matokeo bora zaidi katika mawasiliano na kushirikiana duniani kote. Hali ya kutokuwa na matoleo tofauti ya hati na kuweza kushirikiana kwenye hati katika muda halisi kwenye saa tofauti za maeneo imewafaa zaidi.

“Katika miaka 20 iliyopita, uwiano wa watu walio na lishe duni katika maeneo ambayo hayajaendelea zaidi duniani umepungua kwa takribani asilimia 50. Hili ni jambo la kufurahia. Mafanikio haya yanatokana na usaidizi wa mashirika kama Google. Ushirikiano wetu na Google umetusaidia kupiga hatua kubwa. Nchini Kambodia, tunatumia teknolojia ya Google kutekeleza suluhu ya kudumu ya utapiamlo. Nchini Marekani, tunatumia pia Ruzuku za Google Ad kutoka Google na Google Analytics. Zana hizi husaidia kukuza maarifa bora kwenye utendaji wetu mtandaoni.”

Andrea Tamburini, Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) katika Action Against Hunger

Athari

Mwaka uliopita mipango ya lishe ya Action Against Hunger ilifikia watu milioni 1.51. Katika miaka 10 iliyopita, idadi ya watoto waliopokea matibabu ya utapiamlo mkubwa iliongezeka mara tatu1. Uwekezaji kwenye lishe ni mojawapo wa njia zenye gharama nafuu na inayoleta mabadiliko makuu duniani. Utafiti mpya unaonyesha kuwa kila $1 iliyowekezwa kwenye lishe ya mtoto katika siku 1,000 za kwanza inaleta manufaa ya wastani wa $162. Kuwekeza kwenye lishe huwapa watoto msingi wa maisha yenye afya, matokeo mazuri na hubainisha msingi wa maendeleo ya kudumu duniani kote katika afya na ustawi.

Ruzuku za Google Ad zilivutia watu 158,000 kwenye tovuti yao katika miezi 12 iliyopita na ikachangisha zaidi ya $66,000. Kwa sababu gharama ya kutibu mtoto aliye na utapiamlo ni dola $45 pekee, sasa watoto 1,466 watapata afya bora.

Action Against Hunger imechangisha zaidi ya $20,000 kutoka kwa walioelekezwa kwenye tovuti kupitia YouTube. Idadi hii ilifuatiliwa kupitia kipengele cha kufuatilia cha biashara pepe kwenye Google Analytics. Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida umesaidia Action Against Hunger kutatua changamoto nyingi za nyenzo na hatimaye kuokoa maisha ya wengi.

1. Chanzo: https://www.actionagainsthunger.org/impact/nutrition
2. Chanzo: https://www.actionagainsthunger.org/sites/default/files/publications/Action-Against-Hunger-2015-Annual-Report-web.pdf

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.