Pata maarifa haraka kwa kutumia Google Forms
Tayarisha na ushiriki fomu na hati za utafiti kwa urahisi na uchambue majibu katika muda halisi.
Tayarisha fomu ya mtandaoni kwa urahisi kama tu kutayarisha hati
Chagua kutoka kwenye aina nyingi za maswali, buruta na udondoshe ili upange maswali upya na uweke mapendeleo ya thamani kwa urahisi tu kama kubandika orodha.
Tuma fomu na hati maridadi za utafiti
Weka mapendeleo ya rangi, picha na fonti ili urekebishe mwonekano na muundo au uwakilishe chapa ya shirika lako. Ongeza pia mantiki maalum inayoweza kuonyesha maswali kulingana na majibu, ili kurahisisha matumizi zaidi.
Chambua majibu kwa kutumia mihtasari ya kiotomatiki
Angalia chati zilizo na taarifa kuhusu data ya majibu katika muda halisi. Au ufungue data ghafi ukitumia Google Sheets kwa uchambuzi wa kina au kuiweka kiotomatiki.
Andaa na ujibu tafiti ukiwa mahali popote
Fikia, tayarisha na ubadilishe fomu popote ulipo, ukitumia skrini ziwe ni kubwa au ndogo. Watu wengine wanaweza kujibu utafiti wako wakiwa popote pale—wakitumia kifaa chochote za mkononi, kompyuta kibao au kompyuta.
Tayarisheni fomu na mchambue matokeo pamoja
Ongeza washirika—kama tu kwenye Hati, Majedwali na Slaidi za Google—ili mbuni maswali pamoja katika muda halisi. Kisha, chambueni matokeo pamoja bila kulazimika kushiriki nakala nyingi za faili hiyo.
Tumia data safi ya majibu
Tumia umahiri wa ndani ya programu kuweka sheria za kuthibitisha majibu. Kwa mfano, hakikisha kwamba anwani za barua pepe zimeandikwa kwa muundo unaofaa au kwamba nambari zinapatikana katika safu fulani iliyobainishwa.
Shiriki fomu kupitia barua pepe, kiungo au tovuti
Ni rahisi kushiriki fomu na watu mahususi au na hadhira pana kwa kupachika fomu kwenye tovuti yako au kwa kushiriki viungo kwenye mitandao jamii.
Usalama, utiifu na faragha
Ni salama kwa chaguomsingi
Tunatumia hatua za usalama ambazo ni bora zaidi katika sekta hii ili kuweka data yako salama, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa kina dhidi ya programu hasidi. Fomu za Google zimeundwa mahususi kutumika kwenye wingu, kwa hivyo hakuna haja ya kuweka faili kwenye kifaa na hivyo hupunguza hatari kwenye vifaa vyako.
Usimbaji fiche wakati wa kupitisha na usio wa kupitisha
Faili zote zilizopakiwa kwenye Hifadhi ya Google au zilizoundwa kwenye Fomu za Google husimbwa kwa njia fiche wakati zinapitishwa na wakati hazipitishwi.
Utiifu unaotuwezesha kutimiza matakwa ya sheria
Bidhaa zetu, ikiwa ni pamoja na Fomu za Google, mara kwa mara hupitia uthibitishaji huru wa usalama, faragha na vidhibiti vya utiifu.
Huduma iliyoundwa kwa kuzingatia faragha
Fomu za Google hufuata ahadi madhubuti za faragha na ulinzi wa data, sawa na huduma zingine za Google Cloud kwa biashara.
Unadhibiti data yako.
Hatutumii kamwe maudhui yako ya Fomu za Google kwa madhumuni ya utangazaji.
Hatuuzi kamwe taarifa zako binafsi kwa wahusika wengine.
Tafuta mpango unaokufaa
Google Forms ni sehemu ya Google Workspace
Kila mpango unajumuisha
Kwa Matumizi Binafsi (Bila malipo) |
Business Standard$12 USD
kwa kila mtumiaji kwa mwezi, ahadi ya mwaka 1 Au $14.40 kwa kila mtumiaji kwa mwezi, unapolipia kwa kila mwezi
|
|
---|---|---|
Hati, Majedwali, Slaidi, Fomu za Google
kubuni maudhui |
||
Hifadhi ya Google
Hifadhi salama ya wingu |
GB 15 kwa kila mtumiaji |
TB 2 kwa kila mtumiaji |
Hifadhi za pamoja za timu yako |
||
Gmail
Barua pepe salama |
||
Anwani maalum ya barua pepe ya biashara |
||
Meet
Kufanya mikutano ya video na ya sauti |
Washiriki 100 |
Washiriki 150 |
Rekodi za mikutano huhifadhiwa kwenye Hifadhi ya Google |
||
Msimamizi
Usimamizi chini ya mamlaka moja |
||
Vidhibiti vya sera za usalama kulingana na kikundi |
||
Usaidizi kwa wateja |
Usaidizi wa kujihudumia mtandaoni na majadiliano ya jumuiya |
Usaidizi mtandaoni usiku na mchana, kila siku na majadiliano ya jumuiya |
Piga hatua kwa kutumia violezo
Chagua kwenye violezo mbalimbali vya hati za utafiti, hojaji na violezo vingine vilivyoundwa kitaalamu ili uanze kufanya mambo haraka.
Tembelea Matunzio ya Violezo vya Fomu za Google kwa maelezo zaidi.